
Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Hizbullah ilieleza kuwa shambulio hilo ni ukiukaji mkubwa na usio na kifani wa sheria za kimataifa, ikiripotiwa na Al-Manar. Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa harakati hiyo inalaani uvamizi wa kigaidi na wa kiunyanyasaji wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Venezuela, ikiwemo kulengwa kwa mji mkuu Caracas, miundombinu muhimu, maeneo ya kiraia na makazi, pamoja na kutekwa kwa Rais Nicolas Maduro na mke wake. Hizbullah imesema uchokozi huo wa Marekani dhidi ya Venezuela ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya kitaifa ya nchi huru, sheria za kimataifa na mikataba ya Umoja wa Mataifa kwa visingizio vya uongo.
Hizbullah iliongeza kuwa uvamizi huu ni uthibitisho mpya wa sera za kidhalimu na za kifisadi zinazotekelezwa na serikali ya Marekani bila kujali uthabiti na usalama wa dunia, na kwa lengo la kuimarisha “sheria ya msituni” ili kubomoa mabaki ya mfumo wa kimataifa na kuondoa dhamana yoyote kwa mataifa.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa Marekani, ambayo bado imejawa na wazimu wa kutaka kutawala na kuhodhi, hasa chini ya rais wake wa sasa, inaendeleza sera za uvamizi zinazolenga kuyaweka mataifa huru chini ya satwa yake ya kibeberu, kupora mali na rasilimali zao, na kuendesha vita vya kubadilisha mipango ya kitaifa, huku ikidai kwa uongo kusambaza amani na kuunga mkono demokrasia na uhuru wa mataifa kujiamulia mustakabali wao.
“Hata hivyo, sura yake ya kweli ya kihalifu imefichuka kila mahali, kuanzia Afghanistan hadi Iraq, Yemen, Iran, na kuunda ugaidi kwa mikono ya Marekani pamoja na kuungwa mkono na kibaraka wake, Israel, kama mshirika katika mienendo yake ya kihalifu, ya uvamizi na ya kikoloni. Wakati jumuiya ya kimataifa, badala ya kusimama na kupiga kengele ya hatari dhidi ya uvamizi huu, imechagua ukimya wa aibu. Uvamizi wa leo dhidi ya Venezuela ni tishio la wazi kwa kila taifa huru lisilokubali utawala na utii kwa Marekani.”
Hizbullah ilitangaza mshikamano wake kamili na taifa, urais na serikali ya Venezuela katika kukabiliana na uvamizi huu wa Marekani, ikisisitiza kuwa hatimaye utashindwa mbele ya irada ya watu huru wa Venezuela, taifa lililosimama kupinga kila aina ya ubeberu na ukoloni katika ardhi yake na daima likiunga mkono masuala ya haki na ya waliodhulumiwa duniani, ikiwemo suala la Palestina.
Aidha, Hizbullah imetoa wito kwa mataifa yote, serikali, jamii na makundi huru duniani kulaani uvamizi huu na kusimama pamoja na Venezuela na wananchi wake, kuunga mkono haki ya taifa hilo kujilinda na kutetea uhuru na mamlaka yake ya kitaifa.
3495952
Zenye maoni mengi zaidi