IQNA

Tamasha la kimataifa la ‘Roho ya Unabii’ lazinduliwa Karbala

18:51 - January 02, 2026
Habari ID: 3481755
IQNA-Toleo la nane la tamasha la kimataifa la kitamaduni kwa wanawake, liitwalo ‘Roho ya Unabii’, limezinduliwa mjini Karbala, Iraq, siku ya Alhamisi.

Tamasha hili limehudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi za Kiarabu na nyinginezo, na litadumu kwa siku tatu. Tawi la Shule za Kidini za Wanawake la Kafeel, chini ya usimamizi wa Haram ya Hadhrat Abbas (AS), limeandaa tamasha hili kwa kauli mbiu: ‘Fatima al-Zahra (SA): Kujenga Ufahamu na Kufufua Thamani.’

Kauli mbiu ya toleo hili ni: ‘Fatima al-Zahra (SA) Mkutanisha wa Nuru Mbili: Unabii na Uimamu.’

Sherehe ya ufunguzi ilihudhuriwa na maafisa na wakuu wa idara mbalimbali za Haram ya Abbas (AS), viongozi rasmi, maprofesa wa vyuo vikuu, watafiti na wajumbe wa wanawake kutoka Lebanon, Tunisia, Iran, Afghanistan, Indonesia, Kuwait, Saudi Arabia, Oman na Bahrain.

Ratiba ya ufunguzi ilijumuisha vipengele vya kitamaduni na kisanii vilivyoanza kwa hotuba ya mlezi wa kidini wa haram, Hujjatul-Islam Sayyid Ahmad al-Safi.

Sherehe hiyo pia iliwatunuku heshima familia kadhaa za mashahidi, ili kutambua kujitolea kwao na kusisitiza nafasi yao ya juu katika kumbukumbu ya kitaifa na kijamii.

4326436

captcha