Kongamano hilo litachunguzasuala la kushirikishwa Waislamu katika nyanja zote za kisiasa nchini Uingereza hasa katika matukio ya zama hizi.
Waislamu wamekuwa na nafasi muhimu katika viwango mbalimbali vya siasa za Uingereza na wamewakilishwa katika nafasi mbalimbali za kuchaguliwa tokea Bashir Maan awe mjumbe katika Baraza la Mji wa Glasgow mwaka 1970.
Mafanikio mengine yalikuwa ni Waislamu kushikilia nafasi kama vile meya mwaka 1985, mbunge 1997, na lodi mwaka 1998, waziri mwaka 2007 na mbunge wa kwanza mwanamke Muislamu mwaka 2010. Kwa miaka mingi chama cha Leba kimetawala siasa katika jamii za Waislamu Uingereza lakini sasa Waislamu pia wako katika chama cha Conservative.
Pamoja na hayo Waislamu wamekasirishwa na sera za kimataifa za Uingereza kuhusu masuala kama vile Kashmir, Palestina n.k jambo ambalo limepelekea baadhi kususia kushiriki katika siasa za nchi hiyo.
Nafasi ya misikiti pia imetajwa kuwa muhimu katika maisha ya kisiasa ya Waislamu Uingereza. Hayo ni kati ya masuala yatakayojadiliwa katika kongamano hilo.
914866