Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Kiislamu la Sayansi, Elimu na Utamaduni ISESCO, sherehe hizo katika mji mkuu wa Indonesia zilijumuisha maonyesho ya sanaa na warsha kuhusu umuhimu wa utamaduni wa Kiislamu.
Aidha washirki walipata fursa ya kujifunza kuhusu thamani za mji wa Jakarta na nafasi yake katika turathi za Kiislamu katika fremu ya mabadiliko yaliyoletwa na utandawazi. Aidha mji huo umejadiliwa kama kitovu cha tamaduni, mawasiliano, mazungumzo, kuishi pamoja kwa amani na kiunganishi cha mashariki na magharibi.
Kati ya shughuli za wiki hiyo ni pamoja na maonyesho ya kaligrafia, tamasha ya muziki ya masufi, maonyesho ya sanaa za watoto, maonyesho ya mavazi ya Kiislamu na soko la sanaa za mkono mjini humo.
924528