Kwa mujibu wa gazeti la Al Ahram, Sheikh Uwaiza aliaga dunia katika mji wa Qana kusini mwa Misri akiwa na umri wa miaka 100.
Sheikh Muhammad Uwaiza alikuwa amehifadhi mbinu saba za qiraa ya Qur’ani Tukufu na alitoa mafunzo kwa maqarii wengi wa Misri.
Darsa zake za qiraa aidha zilikuwa mahala pa mkutano wa wanaharakati wa Qur’ani kutoka maeneo mengi ya Misri. Wanafunzi wengi wa vyuo vikuu pia walijifunza tajweed katika darsa zake.
Alifunza qiraa na tajweed ya Qur’ani katika chuo chake cha Darul Qur’ani katika eneo la Ash-Shu’un katika mkoa wa Qana kwa muda wa miaka 50.
929897