IQNA

Mufti Mkuu wa Palestina atembelea Baitul Qur'ani Bahrain

16:57 - January 07, 2012
Habari ID: 2252705
Mufti Mkuu wa Palestina Sheikh Muhammad Hassan ametembelea Baitul Qur'ani katika mji mkuu wa Bahrain, Manama.
Gazeti la al Wasat la Bahrain limeandika kuwa Kasisi Mufid Muslih wa Kanisa la Orthodox la Palestina, Othman Abu Ghariba ambaye ni msimamizi wa faili la Quds Tukufu na Taha Muhammad Abdul Qadir balozi wa Palestina nchini Bahrain walifuatana na Mufti Mkuu wa Palestina katika kukagua Baitul Qur'ani nchini Bahrain.
Ujumbe huo ulitembelea na kukagua kituo hicho cha Qur'ani ambacho ni moja ya nembo za ustaarabu wa Kiislamu nchini Bahrain.
Mufti Mkuu wa Palestina amewashukuru wasimamizi wa kituo hicho cha Qur'ani chenye kumbi 10 kwa kuuita mmoja wa kumbi hizo kwa jina la Quds Tukufu.
Mufti Mkuu wa Palestina, balozi Muhammad Abdul Qadir na mwakilishi wa Kanisa la Orthodox la Palestina wameitaja Baitul Qur'ani ya Bahrain kuwa ni nembo yenye thamani kubwa ya utamaduni wa Kiislamu ambayo inatoa elimu na maarifa kuhusu turathi na historia ya Kiislamu kwa watu wanaoitembelea. 930541


captcha