IQNA

Tafsiri ya al Mizan kutarjumiwa kwa lugha ya Kifaransa

16:59 - January 07, 2012
Habari ID: 2252707
Afisa anayeshughulikia mpango wa kutarjumu tafsiri ya al Mizan kwa lugha ya Kifaransa katika Jumuiya ya Nyaraka na Maktaba ya Taifa ya Iran amesema kuwa tafsiri hiyo itatarjumiwa kwa lugha ya Kifaransa na wataalamu wa tarjumi ya Qur'ani wa vyuo vikuu vya kidini wataalikwa kushiriki katika mradi huo.
Sayyid Muhammad Burhani ameiambia IQNA kwamba tafsiri ya al Mizan iliyoandikwa na mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu Allamah Muhammad Hussein Tabatabai itafasiriwa kwa lugha ya Kifaransa kwa ushirikiano wa Maktaba ya Taifa ya Iran, Jumuiya ya Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu, Taasisi ya Beethat na Chuo Kikuu cha Imam Sadiq (as).
Mhakiki huyo wa masuala ya Qur'ani amesema kuwa kwa sasa tarjumi ya tafsiri ya al Mizan kwa lugha ya Kifaransa iko katika awamu zake za mwanzo na inahitajia muda mrefu. Ameongeza kuwa inakadiriwa kuwa kazi ya kutarjumu tafsiri hiyo kwa lugha ya Kifaransa itachukua kipindi cha miaka 7. 927694





captcha