Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katibu wa baraza hilo Bw. Khabari ameyasema hayo katika mkutano wake na wanachama wa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu katika mji mtakatifu wa Qum.
Amesema kuna wanachuo milioni moja katika taaluma ya sanaa nchini Iran na hivyo kuna haja ya kuratibu shughuli zao za sanaa kwa mtazamo wa Uislamu.
Khabari amesema chuo kikuu cha sanaa za Kiisalmu kitakuwa kituo muhimu cha kutoa mafunzo kwa wasanii wanaofungamana na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
Ameongeza kuwa kuanzishwa chuo hicho ni moja ya masuala yaliyo katika ajenda ya Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni.
930480