IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Dubai kuanza tarehe 21 Januari

14:58 - January 16, 2012
Habari ID: 2257705
Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani, Zawadi ya Dubai, imetangaza kuwa hatua ya mwanzo ya duru ya 13 ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani, Zawadi ya Dubai imeakhirishwa na kusema kwamba sasa yatafanyika tarehe 21 mwezi huu wa Januari.
Awali mashindano hayo yalipangwa kuanza ijumaa iliyopita ya tarehe 13. Taasisi iliyotajwa imesema kuwa sababu ya kuakhirishwa mashindano hayo ni kuwa washiriki wake wengi walikuwa kwenye mapumziko ya muhula wa kwanza wa masomo. Imesema wengi wa washiriki wa mashindano hayo ni wanafunzi.
Sehemu ya mwisho ya mashindano hayo itaanza tarehe 4 Februari na kuendelea kwa muda wa siku 10.
Ahmad Swafar as-Suweidi, mwanachama wa kamati inayoandaa mashindano hayo amesema kuna washindani 264 wanaoshiriki katika hatua ya mwanzo ya mashindano hayo ambapo washindi watapewa fursa ya kushiriki katika hatua ya mwisho. 935439
captcha