Jumuiya ya Walimu na Wasimamizi wa Madrasa za Qur'ani za Senegal ilitoa taarifa jana ikikosoa siasa za serikali ya nchi hiyo kuhusu vituo na madrasa za Qur'ani na kutoa wito wa kutazamwa upya sheria zinazohusiana na shule hizo.
Sehemu moja ya taarifa hiyo imesema walimu wa madrasa za Qur'ani wamekutana mara nyingi na kuzungumza na maafisa wa serikali kuhusu upuuzwaji wa wanafunzi wa vituo vya kidini. Imesema aghlabu ya wanafunzi wa madrasa za Qur'ani wamepuuzwa na serikali na wala hawapewi huduma ya aina yoyote.
Imesema wakati shule za sekta ya binafsi zinafaidika na huduma bora, madrasa za Qur'ani ambazo ziko chini ya serikali zimenyimwa huduma hizo, na watoto wadogo wa Kiislamu wanaopata elimu katika madrasa hizo hawapati msaada wowote wa taasisi za elimu. 939568