IQNA

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Morocco waenziwa

17:20 - January 28, 2012
Habari ID: 2263532
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Morocco yalimalizika jana kwa washindi kutunukiwa zawadi.
Shirika la habari la Kuwait KUNA limeripoti kuwa mashindano hayo yalimalizika jana usiku katika Msikiti wa al Hassan al Thani mjini Casablanca.
Amina Salama kutoka Algeria alishika nafasi za kwanza katika hifdhi ya Qur'ani nzima, tartili na tafsiri katika upande wa wanawake, na katika upande wa wanaume Zakaria Muhammad Ali kutoka Lebanon ameshinda katika hifdhi ya hizbu tano, tajwidi na tafsiri.
Mashindano ya 17 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Morocco yamewashirikisha vijana 41 kutoka nchi mbalimbali za Kiarabu na Kiislamu.
Kamati ya majaji wa mashindano hayo ilijumuisha makari 10 mashuhuri wa kimataifa na wataalamu wa Qur'ani na iliongozwa na Muhammad Jamiil Mubarak kutoka Morocco. 941788

captcha