IQNA

Mashindano ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani kufanyika Ufaransa

10:40 - January 29, 2012
Habari ID: 2263926
Mashindano ya kumi ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 8 Aprili nchini Ufaransa kwa hima ya Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Ufaransa.
Tovuti ya uoif-online imeripoti kuwa mashindano hayo yatasimamiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani Tukufu na Taasisi ya Ulaya ya Sayansi za Jamii na za Kiislamu katika vitengo vya hifdhi ya Qur'ani nzima, juzuu 2, 4, 10, 15 na hizbu 15.
Viongozi wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Ufaransa wanasema kuwa duru ya kumi ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu itafanyika katika sehemu mbili za wanaume na wanawake.
Makari na mahafidhi wa Qur'ani wa miji mbalimbali ya Ufaransa wametakiwa kujiandikisha katika mtandao wa http://www.uoif-online.com.

captcha