Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe hiyo itahudhuriwa na Mohammad Abdulfadhil Alfusi Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Misri. Washiriki 73 wa waliofuzu katika vitengo vya hifdhi watatunukiwa zawadi.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Ahram, duru ya Pili ya mashindano ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu maalumu kwa wenye ulemavu wa kiakili yalifanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa himaya ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Misri.
Waliofanikiwa katika mashindano hayo watatunukiwa zawadi za kifedha katika hafala hiyo.
943229