IQNA

Mashindano ya hifdhi ya Qur’ani kufanyika Uingereza

16:54 - February 08, 2012
Habari ID: 2271479
Mashindano yaa hifdhi na kiraa ya Qur’ani Tukufu yamepangwa kufanyika katika Kituo cha Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithnaashari katika eneo la Stanmore nchini Uingereza. Mashindano hayo yatafanyika kwa hima ya Darul Qur’an wal Itra.
Mashindano hayo yatafanyika katika awamu tano za watoto wenye umri wa miaka 5-8, miaka 9-13, miaka 14-18 na vijana wenye umri wa zaidi ya miaka 18. Vilevile kutakuwepo mashindano ya hifdhi ya juzuu ya kwanza ya Qur’ani Tukufu.
Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kunyanyua juu uwezo wa kisoma Qur’ani kati ya washiriki. Viwango vya washindani vitatathminiwa na majaji wa mashindano hayo kwa kuzingatia kanuni za tajwidi, makharij ya herufi na kadhalika.
Kila mshiriki katika mashindano hayo atapewa dakika tatu za kusoma sehemu ya sura ya Qur’ani itakayochaguliwa na majaji.
Tarehe ya kufanyika mashindano ya utangulizi itatangazwa baadaye na Darul Qur’an wal Itra na washindi wa mashindano hayo ya mwanzo watapata fursa ya kushiriki kwenye awamu ya mwisho ya mashindano hayo. 950099
captcha