Jumuiya ya Maonyesho ya Sanaa ya Kiislamu ya Marekani imewataka wasanii kukabidhi kazi zao kwa taasisi hiyo tarehe 10 na 17 Machi mwaka huu.
Wasanii wanaweza kuonyesha kazi zao zilizotengenezwa kwa ilhamu ya Qur'ani Tukufu katika maonyesho hayo.
Wasanii watoto wenye umri wa kati ya miaka 8 hadi 15 pia wanaweza kushiriki katika maonyesho hayo.
Wakati na mahala maonyesho hayo yatakapofanyika patatangazwa baadaye.
Mwaka uliopita wa 2011 Jumuiya ya Maonyesho ya Sanaa ya Kiislamu ya Marekani (IAE) ilisimamia maonyesho ya "Turath ya Qur'ani, Ujumbe wa Amani" katika miji mbalimbali ya nchi hiyo. 957669