IQNA

Uganda yasisitiza kuwaunga mkono wananchi madhlumu wa Palestina

11:37 - April 05, 2012
Habari ID: 2298154
Serikali ya Uganda imesisitiza juu ya ulazima wa kuungwa mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye amekutana na ujumbe wa bunge la Palestina uliokuweko ziarani Uganda kwa ajili ya kushiriki kwenye kikao cha Umoja wa Mabunge Duniani amesisitiza juu ya ulazima wa kuungwa mkono wananchi madhlumu wa Palestina. Museveni pia amesema kuna ulazima wa kukomeshwa mapigano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Katika mazungumzo hayo, ujumbe wa bunge la Palestina pia umepongeza msimamo wa serikali na wa wananchi wa Uganda kuhusiana na kadhia ya Palestina. Aidha umeitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua mara moja ili kusitisha jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.
Kikao cha 126 cha Umoja wa Mabunge Duniani kinafanyika huko Kampala mji mkuu wa Uganda kuanzia tarehe 31 Machi hadi Aprili 5 mwaka huu ambapo mataifa karibu 160 yanashiriki
captcha