IQNA

Maombolezo ya Bibi Fatma Zahra (as) yafanyika Ujerumani

17:37 - April 29, 2012
Habari ID: 2314504
Maombolezo ya kuuawa shahidi Bibi Fatma az-Zahra (as) binti wa Bwana Mtume (saw) yalifanyika hivi karibuni mjini Ujerumani ambapo wafanyakazi wa ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Wairani na Waislamu wengine wapenzi wa Ahlul Beit (as) wanaoishi nchini humo walishiriki.
Makumbusho hayo ambayo yaliendelea kwa muda wa nyusiku tatu yalimalizika siku ya Alkhamisi usiku katika Kituo cha Kiislamu cha Berlin ambapo wapenzi na wafuasi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) walishiriki kwa wingi.
Ziara ya Bibi Fatma (as), Jamia Kabira na dua ya Kumeil pamoja na swala za jamaa za Maghrib na Ishaa ni sehemu ya ratiba zilizotekelezwa katika nyusiku hizo tatu.
Hujjatul Islam wal Muslimin Hashimiyan alitoa hutuba katika makumbusho hayo ambapo alibainisha na kufafanua sifa na fadhila za Bibi Fatma (as) ambaye ni mbora na kiongozi wa wanawake wa ulimwengu na peponi. Aliwaongoza pia katika kuomboleza kifo cha mtukufu huyo wa Ahlu Beit (as). 995427
captcha