IQNA

Iran yasimamia mashindano ya Qur'ani Zimbabwe

18:22 - May 05, 2012
Habari ID: 2318800
Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Harare katika mji mkuu wa Zimbabwe kimeandaa mashindano ya Qur'ani yaliyofanyika Mei tano.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yalikuwa maalumu kwa vijana na yalikuwa katika vitengo vya hifdhi na qiraa.
Kwa mujibu wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Harare mashindano hayo yamefanyika kwa lengo la kustawisha utamaduni wa Qur'ani miongoni mwa vijana wa Zimbabwe.
Mashindano hayo yamehudhuriwa na viongozi wa Kiislamu Zimbabwe, wanazuoni wa Kiislamu na wanadiplomasia wa nchi za Kiislamu mjini Harare.
Washindi katika mashindano hayo wanatazamiwa kuwakilisha Zimbabwe katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yatakayofanyika Iran kuanzia tarehe 27 Rajab mwaka huu.
1000140
captcha