Akizungumza na IQNA, mwanachama wa Tume ya Qur'ani na Iran katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) ya Iran Sheikh Sayyid Ali Taheri amesema bajeti ya mwaka 1391 Hijria Shamsia (unaoanza 21 Machi 2012 hadi 20 Machi 2013), imeidhinisha Qur'ani ifundishwe katika idara na mashirika mbalimbali ya kiserikali nchini.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa muswada uliopitishwa na Majlisi, serikali inashurutishwa kutumia fedha hizo kwa ajili ya shughuli zinazohusiana na Qur'ani Tukufu.
Sheikh Sayyid Ali Taheri amongeza kuwa bajeti ya shughuli za Qur'ani mwaka huu imeongezwa kwa takribani dola milioni 100.
Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979 shughuli na harakati za Qur'ani zimekuwa zikiimarika kila mwaka. Shughuli hizo zinajumuisha uchapishaji Misahafu, ujenzi wa madrasa za Qur'ani, uandaaji mashindano ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani, utengenezaji programu za kompyuta za Qur'ani n.k
1000835