IQNA

Kongamano la kimataifa la muujiza wa kielimu wa Qur'ani na hadithi za Mtume (saw) laanza

14:06 - May 08, 2012
Habari ID: 2321012
Kongamano la kwanza la kimataifa la muujiza wa kielimu wa Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume (saw) lilianza hapo siku ya Jumapili katika Chuo Kikuu cha Bani Suweif mjini Cairo.
Kwa mujibu wa tovuti ya egynews, kongamano hilo limefunguliwa na Abdallah al Misbah, katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Muujiza wa Kielimu wa Qur'ani na Suna za Mtume (saw) na vilevile as-Sayyid Lutfi mkuu wa chuo kikuu kilichotajwa.
Lengo la kuandaliwa kongamano hilo ni kuchunguzwa utafiti uliofanyika hadi sasa kuhusiana na suala la miujiza ya kielimu ya Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume (saw).
Al Misbah amesema watafiti na wahakiki wa Kiislamu wataendelea kufanya utafiti wao katika uwanja huo ili kuweka wazi miujiza ya kielimu iliyomo kwenye Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume (saw). 1001850
captcha