Gazeti la al Bayan la Umoja wa Falme za Kiarabu limeripoti kuwa baraza hilo litaongozwa na Abdullah al Barak ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa kitengo cha Qur'ani Tukufu cha serikali ya Kuwait na makao yake makuu yatakuwa Kuwait.
Muhammad Abdur Rahman Sultanul Ulamaa ambaye ni mwenyekiti wa kitengo cha uhakiki na utafiti wa kimataifa wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tuzo ya Dubai ameteuliwa kuwa naibu mwenyekiti wa baraza hilo.
Baraza la Waasisi la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani linasisitiza juu ya udharura wa kulindwa misingi na kanuni za baraza hilo katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani na udharura wa wasimamizi wa mashindano hayo kuwa wanachama katika baraza hilo.1004298