IQNA

Duru ya nne ya mashindano ya Qur'ani ya Kituo cha Bibi Rukia (sa) yamalizika

17:42 - May 15, 2012
Habari ID: 2326731
Duru ya nne ya mashindano ya kimataifa ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu ambayo yalikuwa yameandaliwa na Taasisi ya Qur'ani ya Bibi Rukia (sa) na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi kadhaa za Kiislamu ilimalizika hapo siku ya Jumapili katika mji mtakatifu wa Qum, nchini Iran.
Akizungumzia suala hilo, Abdul Jalil al-Makrani Mkuu wa Taasisi ya Qur'ani ya Bibi Rukia (as) amesema mashindano hayo yaliyoanza siku ya Jumamosi yaliwashirikisha Mahafidh na wasomaji Qur'ani mashuhuri kutoka nchi tofauti za Kiislamu zikiwemo Saudi Arabia, Bahrain, Iraq na Iran. Amesema mashindano hayo yamefanyika sambamba na sherehe za kuzaliwa Bibi Fatma az-Zahra (a) ambaye ni binti mpendwa wa Bwana Mtume (saw). Mahafidh walishindana katika hatua tofauti za kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 20, 15, 10 na 5 za Qur'ani Tukufu. Muhammad Abu Soud na Muhammad Ridha Ziara walipewa fursa ya kuwasomea kwa sauti zao za kuvutia washiriki na waalikwa wa mashindano hayo baadhi ya aya za Qur'ani. Washindi wa mashindano hayo walikabidhiwa zawadi nono na zilizoambata na loho za kuwashukuru kutokana na juhudi zao kubwa za kukihudumia kitabu kitakatifu cha Qur'ani. 1007951
captcha