Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyed Mahdi Taghavi, Mkuu wa Shughuli za Qur'ani za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Iran amesema mashindano hayo yatafanyika kuanzia Septemba 12 hadi 16 mwaka huu wa 2012.
Amenongeza kuwa mashindano hayo yatasadifiana na siku za kukumbuka kuuawa shahidi Imam Sadeq AS ambaye katika zama zake Fiqhi ya Kishia iliweza kuenea. Zama za Imamu huyo mtukufu pia zimetajwa kuwa zama za kustawi fiqhi ya Kiislamu. Amesema katika zama za Imam Sadeq AS kulishuhudiwa ustawi mkubwa wa sayansi za Qur'ani na ndio sababu suala la kufanyika mashindano haya katika kipindi cha kumbukumbu ya shahada yake liktailiwa mkazo.
Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyed Mahdi Taghavi ambaye pia ni mkuu wa shirika la habari la IQNA amesema kuwa kuchaguliwa mji wa Tabriz kama mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu kunatokana na sifa zake za kiutamaduni hasa kuwepo vyuo vikuu vya kidini mjini humo na pia kutokana na kuwa mji huo ni makao ya wafasiri na maulamaa wakubwa kama vile Allamah Tabatabai MA. Mji wa Tabriz ni moja kati ya miji ya kihistoria ya Iran na ni mji mkuu wa mkoa wa Azerbaijan Mashariki ulio kaskazini magharibi mwa Iran.
Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyed Mahdi Taghavi amesema mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ni nembo ya umoja wa Kiislamu na ameelezea matumaini yake kuwa mashindano ya mwaka huu yataweza kupelekea kuchukuliwa hatua imara katika uga wa harakati za Qur'ani, kuzalishwa elimu kwa msingi wa Qur'ani ili Waislamu waache kutegemea Wamagharibi katika sayansi za kijamii.
1005872