Warsha hiyo imewashirikisha maelfu ya wanafunzi ambao wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya Qur'ani. Arif Rashid, mtaalamu mashuhuri wa masuala ya Qur'ani nchini Pakistan amefundisha na kutoa hotuba kuhusu kitabu hicho kitakatifu katika warsha hiyo ya siku moja. Chuo cha New Garden Town hutoa huduma mbalimbali zinazohusiana na Qur'ani zikiwemo za masomo ya Qur'ani kwa wale wanaovutiwa na masomo hayo. 1012619