Kikao hicho kilianza kwa kisomo cha Qur'ani kilichosomwa na msomaji Qur'ani wa Kimataifa Sayyid Swadaqat Ali. Kisha kiliendelea kwa hotuba iliyotolewa na Raghib Hussein Naimi, Mkuu wa Chuo cha Kidini cha Naima na mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kisuni wa Pakistan. Amesema usomaji na uzingatiaji wa Qur'ani Tukufu humpa msomaji na msikilizaji wa aya zake uchangamfu na nguvu mpya. Ni vyema kuashiria hapa kwamba chuo cha kidini cha Naima ni moja ya vyuo muhimu vya Kisuni nchini Pakistan. Chuo hicho kiliasisiwa na Sarafraz Hussein Naimi. Chuo hicho ni miongoni vya vyuo vichache vya kidini ambavyo huendeshwa kwa msingi wa kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu na kina uhusiano wa karibu pia na wafuasi wa madhehebu ya Ahlul Beit wa Mtume (saw). Ni kutokana na msimamo wa chuo hicho ndipo magaidi wa Kiwahabi walio na chuki kubwa dhidi ya familia ya Mtume (saw) wakamlenga muasisi wake hivi karibuni na kumuua huko Lahore. Hivi sasa chuo hicho kinaendeshwa na mwanawe, Raghib Hussein Naimi, ambaye pia kama alivyokuwa baba yake anakiendesha kwa msingi wa kuleta umoja na mshikamano baina ya madhehebu tofauti za Kiislamu. 1012616