IQNA

Mashindano ya Qur’ani kwa watoto Russia

9:41 - May 22, 2012
Habari ID: 2331198
Mashindano ya Qur’ani maalumu kwa watoto yamefanyika Mei 20 katika mkoa wa Chelyabinsk nchni Russia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA barani Ulaya, mashindano hayo yamefanyika katika Msikiti wa Chebraqul na kuhudhuria na Waislamu wa eneo hilo.
Sheikh Vugar Akbarov Mufti wa mkoa huo amesema wavulana na wasichana walio na umru wa miaka 10 kutoka Wilaya ya Federali ya Ural ndio walioshiriki katika mashindano hayo. Watoto hao walishindana katika vitengo vya hifdhi na qiraa ya Qur’ani Tukufu kwa kujibu maswali ya jopo la majaji. Mashindano hayo yalitangazwa moja kwa moja kupitia tovuti ya msikiti huo.
1012008
captcha