Mahmoud Hussein Hashimi, mwambata wa masuala ya utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Falme za Kiarabu Imarati, amesema kuwa Iran itawakilishwa hivi karibuni katika duru ya 29 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu, Zawadi ya Dubai ambayo imepangwa kufanyika nchini humo tarehe 18 Juni.
Mashindano hayo yatafanyika sambamba na maadhimisho ya kubaathiwa Mtume Mtukufu (saw) hapo tarehe 27 Rajab. Mwaka uliopita pia Iran iliwakilishwa kwenye mashindano hayo na Mahdi Khatibi. Hashimi amesema kuna uwezekano wa waamuzi wa Qur'ani wa Iran kushiriki kwenye duru zijazo za mashindano hayo. Hashimi pia amefanya mahojiano na televisheni ya Dubai ambapo amebainisha nafasi muhimu ya Iran katika kueneza mafundisho, maarifa hifdhi na usomaji wa Qur'ani Tukufu.1012515