IQNA

Kuhifadhi Qur'ani utotoni huwa na athari bora zaidi

12:24 - May 26, 2012
Habari ID: 2334126
Kuhifadhi Qur'ani utotoni ni njia muafaka zaidi na imekuwa ikitumiwa kwa muda mrefu nchini Nigeria, amesema Mhariri Mkuu wa Jarida la Al-Mizan la mjini Zaria katika jimbo la Kaduna Kaskazini mwa Nigeria.
Akizungumza na IQNA, Ibrahim Musa amesema: 'Watoto hapa huanza kuhifadhi Qur'ani wakiwa na umri wa miaka minne, wakati wanapoweza kuzungumza na kudiriki mambo. Wale wenye uerevu wa hali ya juu huanza wakiwa na umri wa miaka mitatu. Pamoja na hayo kuna wale ambao huanza kuhifadhi Qur'ani wakiwa watu wazima, lakini ni wachache.'
Amesema katika vyuo vya Qur'ani Nigeria, kuna mbinu mbali mbali ambazo hutumika kufunza na kuhifadhi Qur'ani. Amesema: 'Katika chuo change kijulikanacho kama Chuo cha Kiislamu cha Fudiyya, darsa hizo zimegawanywa kwa mujibu wa makundi ya umri na kila kikao cha darasa huanza kwa kisomo cha Qur'ani Tukufu'.
Amesema kuwa kote Nigeria na hasa Kaskazini mwa Nigeria, mbinu ya kutoa mafunzo ijulikanayo kam Almajiri Tsangaya hutumika. 'Katika mfumo huu mtoto mwenye umri wa miaka minne hukabidhiwa Malam (mwalimu) hadi pale atakapohifadhi Qur'ani au kufika umri wa miaka 18,' ameongeza.
Ibrahim Musa mwenye umri wa miaka 45 amekuwa mhariri wa jarida la Kihausa la Al Mizan kwa muda wa miaka 20. Jarida hilo linachapishwa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Yakub Zakzaki.
1002009
captcha