Kwa mujibu wa tovuti ya isna.net mashindano hayo ni seehemu ya ratiba zilizopangwa kutekelezwa na Jumuiya ya Waislamu ya Marekani Kaskazini, pambizoni mwa mkutano wake wa kimataifa wa kila mwaka. Mashindano hayo yatafanyika kwa madhumuni ya kuwashajiisha watoto na vijana wa Kiislamu wa Marekani kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Watoto walio na chini ya umri wa miaka 16 watashindana katika makundi matatu ya kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 15 zinazofuatana na juzuu tano pia zinazofuatana. Usomaji pia utafanyika katika makundi mawili ya washindani walio na umri wa chini ya miaka 11 ambapo watatakiwa kusoma Qur'ani nzima huku wakichunga sheria za tajwidi na kundi la pili lililo na umri wa chini ya miaka saba litatakiwa kusoma Qur'ani nzima kwa kisomo cha kawaida. Mbali na mashindano hayo ya Qur'ani maonyesho ya sanaa, filamu na picha za Kiislamu, huduma za tiba ya Kiislamu, tamasha la watoto na ratiba za burudani ya Kiislamu ni miongoni mwa ratiba zitakazotekelezwa pambizoni mwa mashindani hayo. Jumuiya ya Kiislamu ya Marekani Kaskazini ISNA, inayoandaa mashindano na mkutano huo wa kila mwaka inajumuisha mashirika na taasisi mbalimbali za Kiislamu ambazo hujishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii, kimasomo na kiutamaduni kwa lengo la kuhudumia jamii ya Kiislmu ya Marekani. 1016705