IQNA

Hatua ya mwisho ya mashindano ya kitaifa ya Morocco kufanyika

18:57 - May 26, 2012
Habari ID: 2334490
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco imetangaza kuwa itaandaa hatua ya mwisho ya mashindano ya kitaifa ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la Mfalme Muhammad VI hapo tarehe 4 Agosti.
Kwa mujibu wa tovuti ya oujda-portail Wizara hiyo imesema kuwa mashindanohayo yatafanyika katikati ya mwezi wa Ramadhani katika Msikiti wa as-Sunna mjini Rabat mji mkuu wa nchi hiyo. Sherehe za kuhitimisha mashaindano hayo zitafanyika tarehe 8 Agosti. 1016592
captcha