IQNA

Nakala za Qur’ani kusambazwa katika shule Uingereza

12:57 - May 27, 2012
Habari ID: 2334948
Waziri wa Elimu Uingereza Michael Gove amesema itakua jambo bora iwapo wafadhili wataunga mkono mpango wa kutuma nakala za Qur’ani Tukufu katika shule nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Telegraph la London, Gove ambaye amekuwa akiunga mkono usambazwaji Bibilia katika shule za Uingereza amesema wizara yake inatafakari suala za ‘kusambaza vitabu vingine vitakatifu kama Qur’ani katika shule za nchi hiyo. ‘Iwapo watu watawasilisha mapendekezo, wafadhili na wengine, basi tunaweza kusambaza nakala za Qur’ani katika shule’, amesema waziri huyo.
Katika siku za hivi karibuni wizara ya elimu Uingereza ikishirikiana na wafadhili Wakristo wamesambaza nakala 24 za Bibilia katika shule za nchi hiyo.
1017502
captcha