IQNA

Qur'ani kupewa kipaumbele zaidi katika bunge jipya la Iran

12:57 - May 27, 2012
Habari ID: 2335058
Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (bunge) amba italipa kipaumbele zaidi suala la kuimarisha utamaduni wa Qur'ani nchini.
Hayo ni kwa mujibu wa Sheikh Sayyed Mohammad Baqer Ebadi akizungumza na IQNA amesema ustawishaji wa utamaduni wa Qur'ani na hasa madrasah za Qur'ani ni suala ambalo litapewa umuhimu mkubwa katika awamu ya tisa ya bunge la Iran ambalo limeapishwa leo.
Sheikh Ebadi amesisitiza kuwa haitoshi kuisoma na kuihifadhi Qur'ani kwani utamaduni wa Qur'ani unapaswa kuingia katika maisha ya Waislamu.
Ameashiria pia kuhusu umuhimu wa vyuo vikuu vya Kiislamu na kuongeza kuwa kunahitajika mikakati ya kuunga mkono vyuo hivyo kwani vina nafasi muhimu katika jamii. Mbunge huyo pia ametaka zizidishwe harakati za utamaduni zenye lengo la kustawisha masuala ya hijabu na kujistiri.
1016580
captcha