IQNA

Kikao cha kuchunguza katiba mpya ya uchapishaji Qur'ani nchini Misri kufanyika

18:04 - May 27, 2012
Habari ID: 2335369
Baraza la Sekta ya Uchapishaji na Ufungaji ya Misri imeelezea matayarisho ya kufanyika kikao cha kuchunguza sheria mpya ya uchapishaji na usambazaji wa Qur'ani Tukufu nchini humo ambapo Sheikh wa al–Azhar anatazamiwa kushiriki.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Yaum as-Sabe, linalochapishwa nchini Misri baraza hilo limetangaza kuwa linaafikiana na sheria hiyo mpya na kwamba litatuma ujumbe wa wanachama wake kwenda kujadiliana suala hilo na Ahmad Tayyib, Sheikh wa al-Azhar. Kikao hicho kitajadili sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa watu wanaopotosha Qur'ani na kuichapisha bila kibali kutoka wa idara husika za Misri. Wanachama wa sekta iliyotajwa wamesema kuwa watataka kubainishwa vyema kwa maana halisi ya neno 'upotoshaj' na pia kutolewa kwa suhula zinazohitajika kwa ajili ya kuyawezesha mashirika ya uchapishaji Qur'ani kuchapisha kitabu hicho cha mbinguni bila makosa. Wamesema kama kikao chao na Sheikh Ahmad Tayyib hakitafanikiwa kufikia natija ya kuridhisha watatafuta njia zingine za kufikia malengo yao kupitia Muungano wa Wachapishaji na Viwanda vya Uchapishaji Qur'ani.
Tunakumbusha hapa kwamba tarehe 8 Mei Kamisheni ya Mapendekezo na Malalamiko ya Bunge la Misri ilipasisha kifungo cha kati ya miaka 10 hadi 15 jela na faini ya fedha kwa watu watakaopatikana na kosa la kupotosha Qur'ani. 1016945
captcha