Kongamano hilo limehudhuriwa na wanazuoni, wasomi, wanafikra na shakhsia mashuhuri wa Kishia na Kisuni kutoka pembe zote za Pakistan. Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kuwaunganisha Waislamu wa madhehebu za Kiislamu. Katika kongamano hilo Hujjatul Islam wal Muslimin Nassir Abbas Jaffar Katibu wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu wa Pakistan na pia Muhammd Amin Shahidi naibu katibu wa majlisi hiyo walitoa hutuba na kuzungumzia malengo ya kuandaliwa kongamano hilo pamoja na ratiba zake. Wamesema kongamano hilo limeandaliwa kwa madhumuni ya kuimarisha mwamko na umoja wa Kiislau miongoni mwa Wapakistan. 1017514