IQNA

Tarjumi za Qur'ani Tukufu zaonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu nchini Iraq

12:02 - May 28, 2012
Habari ID: 2335928
Muskha za Qur'ani Tukufu, tarjuma zake na mapambo mbalimbali ya kitabu hicho kitakatifu yanaonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu yaliyopewa jina la Jawadain (as) huko katika mji wa Kadhimain nchini Iraq.
Akibainisha suala hilo, Mushtaq Talib Anad msimamizi wa maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na Idara ya Haram Takatifu ya Imam Musa Kadhim (as) yanafanyika kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Imam huyo mtukufu. Amesema wachapishaji kutoka zaidi ya nchi 60 duniani zikiwemo Iran, Uingereza, Misri, Jordan, Lebanon na Syria zinashiriki katika maonyesho hayo ambapo zinawasilisha vitabu katika nyanja mbalimbali za kidini, kiutamduni na kilugha. Tarjumi za Qur'ani Tukufu katika lugha tofauti za dunia zimewavutia wengi wanaoyatembelea maonyesho hayo. Amesema mbali na vitabu hivyo kuna vibanda maalumu ambavyo vimetengwa kwa ajili ya vitabu vya watoto. Tunaashiria hapa kwamba maonyesho hayo ambayo yalifunguliwa mjini Kadhimain Jumatano tarehe 23 chini ya anwani ya 'Imam Musa bin Jaafar, Chanzo cha Msamaha wa Milele kwa Wanadamu,' yametembelewa na wanafikra, wanazuoni na wasomi wa kidini, kiutamaduni, kisiasa na wawakilishi wa maeneo matakatifu kutoka pembe zote za Iraq. Maonyesha hayo yamepangwa kuendelea hadi Ijumaa Juni Mosi. 1017928
captcha