Sherehe za kufunga mashindano hayo zitafanyika katika Taasisi ya Masomo ya Kiislamu mjini Muscat. Kwa mujibu wa tovuti ya Oman Observer, washindi wa mashindano hayo watatangazwa na Habib bin Muhammad ar-Riyami, Katibu Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Sultan Qabus ambacho ndicho kimeyadhamini. Mashindano hayo yamefanyika katika makundi matano ya hifdhi na tajwidi ya Qur'ani nzima, hifdhi na tajwidi ya juzuu 24, hifdhi na tajwidi ya juzuu 18, hifdhi na tajwidi ya juzuu 12 na hifdhi na tajwidi ya juzuu 6 zinazofuatana za Qur'ani Tukufu. Hatua ya mwanzo ya mashindano hayo iliwashirikisha washindani 285 ambapo hatimaye washindi 142 walichaguliwa kushiriki katika hatua ya mwisho. Washindi wa hatua hii ya fainali na wazazi wao wataenziwa na kutunukiwa zawadi katika sherehe maalumu zitakazofanyika baadaye hii leo. Mashindano hayo hufanyika kila mwaka. 1018414