Mashindano hayo ya 16 yaliandaliwa na Jumuiya ya Jordan ya Ulinzi wa Qur'ani. Washindani 5257 walishiriki katika mashindano hayo ya kitaifa ambapo 3767 kati yao walichaguliwa kuwa washindi wa mwisho. Katika sherehe hiyo Muhammd al-Majali naibu mkuu wa jumuiya iliyotajwa alibainisha shughuli za jumuiya hiyo pamoja na vituo na taasisi nyingine za Qur'ani zinazofungamana nayo. Aya kadhaa za Qur'ani na kasida zilisomwa kwenye sherehe hiyo pamoja na kuonyeshwa filamu fupi ya maisha ya Sheikh Abdallah al-Matu. Licha ya washindi kupewa zawadi pia walitunukiwa loho za kuwashukuru kutokana na juhudi zao kubwa za kuhudumia kitabu hicho kitakatifu. 1019663