Kongamano hilo lilofanyika chini ya kauli mbiu ya 'Kwa Ajili ya Taasisi Endelevu za Qur'ani,' lilizishirikisha taasisi na vituo vya Qur'ani 40 kutoka mikoa tofauti ya Yemen. Akizungumzia kongamano hilo Swaleh ad-Dhibyani, mkuu wa taasisi iliyotajwa amesema kuwa lengo la kuzikutanisha taasisi hizo za Qur'ani ni kuandaa uwanja wa kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na shughuli za vituo hivyo vya Qur'ani nchini Yemen pamoja na kuimarisha ushirikiano kati yao. Amesema shabaha ya mwisho ni kuviwezesha vituo hivyo kuwa na msimamo na pia mbinu moja kuhusu misingi ya utafiti katika vituo hivyo. Amesema kongamano hilo limefanyika katika fremu ya kauli mbiu ya mwaka huu ya jumuiya iliyotajwa ambayo ni; Tuwekeze katika Maisha ya Qur'ani.' Ad-Dhibyani amesema sherehe za kutunuku na kuenzi kundi la 17 la washindi vijana wa kiume wa hifdhi ya Qur'ani na kundi la nne la mabinti mahafidh wa Qur'ani ambao ni watu 120, zitafanyika mwishoni mwa mwezi ujao wa Juni katika ukumbi wa jumuiya hiyo iliyoanzishwa nchini Yemen mwaka 2010. Jumuiya hiyo hujishughulisha na masuala ya mafunzo ya Qur'ani na dini. 1018593