IQNA

Mnara wa Milad Tehran mwenyeji wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani

15:22 - June 02, 2012
Habari ID: 2339376
Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yatafanyika katika ukumbi mkubwa wa Mnara wa Milad mjini Tehran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yatafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mnara kati ya tarehe 17 na 22 Juni.
Sherehe za ufunguzi zinatazamiwa kufanyika Jumapili Juni 17 sambamba na tarehe 27 Rajab ambayo ni siku ya kukumbuka Mab’ath (kubaathiwa) Mtume Muhammad SAW.
Wawakilishi kutoka nchi za Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu watashindana katika vitengo vya hifdhi na qiraa ya Qur’ani Tukufu katika mashindano hayo ya siku sita ambayo yameandaliwa na Shirika la Awqaf la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Pembizoni mwa mashindano hayo kutafanyika kongamano la masomo ya Qur’ani. Maudhui kuu ya kongamano la mwaka huu ni ‘Qur’ani na Mwamko wa Kiislamu’ na ‘ Qur’ani na Mabadiliko ya Jamii ya Mwanaadamu.’
1021415
captcha