Kwa mujibu wa tovuti ya Bernama mashindano hayo yaliyofanyika chini ya anwani ya 'Umoja wa Kiislamu' yaliwashirikisha washiriki 27 kutoka majimbo yote ya nchi hiyo. Katika siku ya kwanza ya mashindano hayo ya kitaifa, wasomaji wawili wa Qur'ani waliwafariji hadhirina kwa kuwasomea visomo vya kuvutia vya aya za kitabu hicho cha mbinguni. Mashindano hayo yataendelea kwa muda wa siku tano ambapo mwishoni washindi watachaguliwa kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya kiraa ya Qur'ani ambayo yanatazamiwa kuandaliwa nchini humo hivi karibuni. Akizungumza mwanzoni mwa mashindano hayo, Najib bin Tun Haji Abdul Razzaq, Waziri Mkuu wa Malaysia amesisitiza juu ya kuzingatiwa umoja miongoni mwa Waislamu bila kuzingatia rangi na makabila yao. Amesema serikali ya Malaysia inafanya juhudi za kuimarisha mafundisho ya Kiislamu katika pembe zote za nchi hiyo kwa sababu hiyo ndiyo dini rasmi nchini humo.1023118