Kwa mujibu wa gazeti la Arab News, Hassanat Bint Ali al-Hureithi ambaye ni mwanafunzi katika Jumuiya ya Hifdhi ya Qur'ani Tukufu mjini Madina anatazamiwa kuiwakilisha Saudi Arabia katika mashindano hayo. Akizungumzia suala hilo, Mansur al-Masih, Katibu Mkuu wa Sekritarieti ya Mashindano ya Qur'ani katika Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia amesema wizara hiyo imechukua uamuzi wa kumtuma binti huyo kwenye mashindano hayo baada ya kupokea mwaliko kutoka kwa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan. Amesena kushiriki kwa mwanamke huyo wa Saudia katika mashindano hayo kutawapa wanawake wengine wa nchi hiyo moyo na hamu zaidi ya kujihusisha na masuala ya Qur'ani. 1024298