Kongamano hilo litakalofanyika kwa madhumuni ya kuchunguza matatizo ya tarjumi ya Qur'ani katika eneo la Asia Pacific litafanyika kwa ushirikiano wa chuo hicho, Taasisi ya Uhakiki wa Kiislamu na Taasisi ya Kimataifa ya Iqbal kwa ajili ya Utafiti na Mazungumzo IRD. Historia ya tarjumi za Qur'ani, uchambuzi wa wa tarjumi zilizoandikwa kwa lugha tofauti za Asia Pacific, athari za madhehebu za Kiislamu katika tarjumi za Qur'ani na matatizo yanayotokana na tarjumi zinazotarjumiwa kutoka lugha zisizo za Kiarabu ni miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo. Kongamano hilo linalotazamiwa kufanyika mapema mwakani, linapokea makala kuhusiana na masuala yatakayojadiliwa kwa lugha mbili tatu za Kiurdu, Kiarabu na Kiingereza. 1025034