IQNA

Duru za mafunzo ya Qur'ani kwa Waislamu wapya nchini Imarati

18:23 - June 10, 2012
Habari ID: 2343722
Masomo ya muda mfupi ya kiraa, hifdhi na tafsiri ya Qur'ani Tukufu yametolewa kwa Waislamu wapya katika Kituo cha Darul Birr katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa Khaleejtimes, Khalid Sultan al-Ulama, mkuu wa kituo kilichotajwa amesema masomo hayo yametolewa sambamba na kuwafundisha washiriki hadithi za Mtume Mtukufu (saw) na vilevile lugha ya Kiarabu. Waislamu wapya 150 wamehudhuria masomo hayo. Sultan ameongeza kuwa watu 750 walifanikiwa kusilimu mwaka huu katika kituo hicho ambapo wameonyesha hamu kubwa ya kuujua Uislamu na mafundisho ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani. Amesema kufikia mwishoni mwa mwaka huu idadi ya watu waliosilimu katika kituo hicho inatazamiwa kuongezeka na kupindukia ya miaka mitatu iliyopita, ambapo kwa utaratibu ilikuwa kama ifuatavyo: 1059, 1500 na 1380. Ameongeza Waislamu hao wapya waliosilimu hivi karibuni wanatoka katika nchi 16 za dunia zikiwemo za Ufilipino, India, China, Uingerea, Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Romania na Russia, ambapo Wafilipino wanaunda asilimia 80 ya Waislamu hao wapya. 1026586
captcha