IQNA

Semina ya uchapishaji Qur'ani kufanyika Madinah

17:16 - June 12, 2012
Habari ID: 2344222
Wizara ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu nchini Saudi Arabia imeandaa semina ya kimataifa kuhusu uchapishaji wa Qur'ani mjini Madina.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, semina hiyo yenye anwani ya 'Uchapishaji Qur'ani: Uhakika na Matarajio' itasimamiwa na Shirika la Uchapishaji Qur'ani la Mfalme Fahd.
Waziri wa Masuala ya Kiislamu na Wakfu nchini Saudi Arabia Saleh Al Sheikh amesema wanazuoni wa ngazi za juu wa Kiislamu, wanaakademia, na wataalamu wa uchapishaji watashiriki katika vikao kadhaa vya semina hiyo.
Waziri huyo amesema washiriki watajadili mada tano kuu ambazo ni: 'Historia ya Uchapishaji Qur'ani', 'Masuala ya Kisayansi katika Uchapishaji Qur'ani', 'Masuala ya Kiufundi katika Uchapishaji Qur'ani', 'Vifaa Vinavyotumika katika Uchapishaji Qur'ani' na 'Mbinu za Kiteknolojia katika Uchapishaji Qur'ani.' Aidha washiriki watajadili juhudi zinazofanywa na Shirika la Uchapishaji Qur'ani la Mfalme Fahad katika kuchapisha na kusambaza Qur'ani Tukufu.
1027199
captcha