IQNA

Darsa za Qur'ani kwa madereva wa taxi Dubai

18:57 - June 11, 2012
Habari ID: 2344237
Madereva wa taxi mjini Dubai nchini Imarati watapewa mafunzo ya Qur'ani kwa lengo la kuboresha maadili yao.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mpango huo ni natija ya juhudi za pamoja za Shirika la Taxi la Dubai DTC na Halmashauri ya Barabara na Uchukuzi RTA. Mpango huo unatazamiwa kuwezesha madereva kuwa na maadili mema na subira wakati wa kazi kutokana na kuwa madereva hao wamekuwa wakituhumiwa kuwa wana utovu wa nidhamu na maadili ya Kiislamu.
'Tunatumia njia ya mafundisho ya Qur'ani Tukufu kujaribu kufikia hisia za nafsi zao ili watafakari juu ya aya zinazohusua muamala wa mwanaadamu', amesema Yusuf Al Ali Mkuu wa DTC.
'Mafunzo haya ya Qur'ani hatimaye yatawawezesha kuwajibika katika vitendo vyao na kuimarisha uhusiano wao na wengine. Madereva wote watapata mafundisho haya pasina kujali dini yao kwani mafundisho ya Qur'ani Tukufu yataathiri vizuri mitazamo na maisha yao.'
1027235
captcha