Masomo hayo maalumu yatakayohusu jinsi ya kuzingatia taratibu na nidhamu na vilevile kuwa na subira wakati wa utekeleaji majukumu yao, yatatolewa kwa mara ya kwanza kwa madereva ambao wamekuwa wakituhumiwa na wasafiri kuwa hawaheshimu misingi ya tabia za Kiislamu wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Akibainisha suala hilo Yusuf Aal Ali mkurugenzi mwandamizi wa Shirika la Teksi la Dubai amesema kuwa kupitia mafunzo hayo ya Qur'ani wana lengo la kuwasaidia madereva wa teksi kunufaika na aya za kitabu hicho cha mbinguni na hasa aya zinazohusiana na utu wa mtu kuboresha uhusiano wao na wasafiri.
Aal Ali amesema masomo hayo yatatolewa kwa wafanyakazi wote wa shirika hilo bila kujali dini zao kwa sababu mafundisho ya Qur'ani Tukufu yana athari kubwa kwa tabia na maisha ya wanadamu wote. 1027277