Katika kikao hicho pande mbili hizo zimeahidi kushirikiana kwa madhumuni ya kuunda kwa pamoja kamati ya kitaalamu itakayoshughulikia sheria hizo ambazo baadaye zitapitishwa na al-Azhar. Washiriki wa kikao hicho wamesema kwamba Qur'ani zitakazochapishwa kwa ruhusa ya kamati hiyo zinapaswa kuwa za kiwango cha juu kiasi kwamba makosa ya chapa hayapasi kupatikana humo. Kamati itakayobuniwa pia itakuwa na jukumu la kuainisha maana halisi ya neno 'upotoshaji' katika uchapishaji wa aya na maneno ya Qur'ani na pia kuanisha adhabu inayopasa kutolewa kuhusiana na viwango mbalimbali vya upotoshaji huo. Sheikh wa al-Azhar amesisitiza udharura wa kutatuliwa matatizo yaliyopo kote nchini kuhusiana na uchapishaji wa kitabu hicho cha mbinguni. 1027183