IQNA

Nchi 65 kushiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Iran

17:02 - June 12, 2012
Habari ID: 2345285
Mkuu wa Shirika la Awqaf la Iran amesema wawakilishi wa nchi 65 kutoka nchi za Waislamu na zisizokuwa za Waislamu watashiriki katika awamu ya 29 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran.
Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran Jumatatu Juni 11, Hujjatul Islam Ali Mohammadi ameongeza kuwa mwaka huu washiriki ni kutoka mabara matano ya dunia.
Sheikh Mohammadi ambaye pia ni mkuu wa Kamati Kuu ya Mashindano ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mashindano hayo yataanza Jumatatu Juni 18 sambamba na sherehe za Mab'ath.
Ameongeza kuwa jopo la majaji lina wanachama 14 ambapo watano ni Wairani na waliosalia ni kutoka nchi mbalimbali duniani.
Katika mashindano ya mwaka huu, wanawake ambao wanajishughulisha na harakati za Qur'ani wataenziwa. Aidha kutakuwa na kongamano la kitaalamu la masuala ya Qur'ani ambapo tayari makala 550 zimewasilishwa.
Mashindano hayo ya Qur'ani yataanza Juni 18 hadi 23 katika Ukumbi wa Mnara wa Milad mjini Tehran.
1027572
captcha