IQNA

Maqarii mashuhuri wa Misri watarajiwa Tehran

17:00 - June 12, 2012
Habari ID: 2345320
Maqarii mashuhuri wa Misri Dr. Ahmed Ahmed Noaina na Ali Mahmoud Shamis wanatazamiwa kuwasili katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wiki ijayo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maqarii hao watakuwa mjini Tehran kuhudhuria Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu na vilevile kushikiriki katika hafla za qiraa ya Qur'ani katika mikoa kadhaa ya Iran.
Kati ya mikoa hiyo ni Tehran, Sistan na Baluchistan pamoja na Khorasan Razavi. Aidha Noaina na Shamis watatoa mafunzo ya Qur'ani katika kipindi watakachokuwa Iran.
Mashindano hayo ya Qur'ani yataanza Juni 18 sawia na 27 Rajab kwa mnasaba wa kubaathiwa Mtume SAW na kuendelea hadi 23 katika Ukumbi wa Mnara wa Milad mjini Tehran.
1028039
captcha