Hayo yamesemwa na mwanaharakati wa Qur'ani na mwandishi wa habari wa Senegal Abu Bakar Diyasi katika mahojiano yake ya shirika la habari la IQNA. Ameongeza kuwa mahafidhi wa Qur'ani nchini Senegal wanatumia mbinu mbalimbali za kwao binafsi au mbinu nyingine maarufu zilizoarifishwa na maqarii wa kitabu hicho. Amesisitiza kuwa madrasa za hifdhi ya Qur'ani ndizo ambazo huainisha mbinu inayotumiwa na wanafunzi wao katika kazi hiyo.
Ustadh Abu Bakar Diyasi amesema kuwa mbinu iliyoenea zaidi katika misikiti na vituo vya Qur'ani nchini Senegal ni ile iliyobuniwa na Abdulmuhsin al Qasim, khatibu na imamu wa Msikiti wa Mtume mjini Madina.
Mwanaharakati huyo wa Qur'ani amesifu mbinu hiyo na kusema inagawa sura za Qur'ani katika sehemu tatu ambazo kila sehemu moja ina juzuu 10. Amesema kuwa mahafidhi huhifadhi ukurasa mmoja wa Qur'ani kila siku na katika siku ya pili hukariri ukurasa huo kabla ya kuanza kuhifadhi ukurasa mwingine. Sifa muhimu zaidi ya mbinu hii ni kukariri na kufanya mazoezi mengi.
Ustadh Diyasi amesisitiza kuwa wenzo muhimu kwa ajili ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu ni kutokata matumaini na kuongeza kuwa, iwapo hafidhi atavunjika moyo kuhusiana na kiwango cha kuhifadhi kwake aya za kitabu hicho au kutokana na kusahau baadhi ya aya, hapana shaka kwamba hawezi kufanikiwa. Amekutaja pia kumtegemea Mwenyezi Mungu Manani, kujiepusha na dhambi na kuwa na matumaini kwamba Qur'ani itafungua njia vinaboresha na kurahisisha kazi ya kuhifadhi maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. 1029120